TIMU za soka za Yanga na Singida United zimezidi kuibomoa Simba baada ya jana kuwasajili wachezaji wake wawili nyota.
Yanga ilimtambulisha mshambuliaji Ibrahim Ajib iliyemsajili kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika. Singida United imemsajili mshambuliaji Pastory Athanas aliyedumu miezi sita tangu ajiunge kutoka Stand United Shinyanga.
Ajib amesaini mkataba wa miaka miwili kukipiga Jangwani na alikabidhiwa jezi namba 10 aliyokuwa akivaa Antony Matheo ambaye hatakuwepo tena Yanga msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika Jezi namba 10 ndiyo ilikuwa ikivaliwa na mshambuliaji wa zamani, Jerry Tegete.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alisema Ajibu hajapotea bali ameenda mahali sahihi. Alimtaka aoneshe jitihada kubwa kutimiza malengo yake. “Ajib ni kijana wangu, hapa hajapotea.
Nimwombe tu kwamba aonyeshe jitihada, nidhamu na pia kiwango bora,” alisema. Mkwasa alisema Ajib akionyesha juhudi na kupata timu zinazomuhitaji nje ya nchi, watamwachia aende kujaribu bahati yake.
Katika hatua nyingine, Klabu hiyo imesema inatarajia kuwapima afya wachezaji wote kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya soka Tanzania bara kuanzia Jumatatu ijayo. Meneja wa Yanga, Hafidh Salehe alisema Kocha George Lwandamina ameagiza wachezaji wapimwe afya ili kujua hali zao waanze maandalizi wakiwa na nguvu
.
AJIBU HUYU HAPA ENZI ZA MSIMBAZIAlisema baadhi ya wachezaji waliokuwa likizo wanawasili leo. Hao ni Thaban Kamusoko na Donald Ngoma wa Zimbabwe. Awali Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo alisema Pastory amesaini kujiunga nao kwa mkataba wa miaka miwili
.
Amesema usajili huo ni pendekezo la Kocha wao Mkuu, Mholanzi Hans van der Pluijm anayemhusudu kutoka Stand United. Sanga ni mchezaji wa pili kuondoka Simba baada ya Ibrahim Ajib kusaini pia mkataba wa miaka miwili na mahasimu, Yanga SC
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}