site to read
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_sl0bYptDlNG591cRHVeQ19EMmwYsn7suAnHDl6D6-4BsrfZEE9rv8CJIVcIDRnKzxXtt4RbL0t1y0LRN_JAUHsc8cxDd3cb0xiIDJpdh_G_jVTLzv6UITsF9P1djgYoJ2xB1tnAm2aH5fqz-Cf7yIwUuHkRzIfjhpc0hKUdc_oEcx3F1D91f6lcw=s0-d)
Dar es Salaam. Uchaguzi wa Chama cha Soka la
Wanawake (TWFA), sasa utafanyika Dar es Salaam badala ya Dodoma na
Morogoro - mikoa iliyotangazwa awali.
Mwenyekiti Kamati
ya Uchaguzi ya TWFA, Wakili George Mushumba, amesema kwamba taratibu
zote zimekamilika na kwamba siku ya uchaguzi ni Jumamosi Julai 8, mwaka
huu.
Wakili Mushumba ametoa wito kwa wajumbe wote
kufika Dar es Salaam Ijumaa Julai 7, mwaka huu kwa ajili ya kufahamu
tararibu za awali za uchaguzi.
Tayari Kamati ya Mushumba ilitangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu.
Majina
yayopitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Theresia
Mung’ong’o, Hilda Masanche, Salma Wajeso, Zena Chande, Triphonia Temba,
Mwamvita Kiyogoma, Jasmine Soudy na Chichi Mwidege.
Nafasi
zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu
Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne
wa Kamati ya Utendaji.
FOMU ZA KUWANIA UONGOZI TAFCA
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania
(TAFCA), Ramadhani Mambosasa ametoa wito wa walimu wa soka kujitokeza
kwa wingi kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi ngazi ya taifa.
Mambosasa ametoa wito huo ikiwa
zimebaki siku mbili tu kwa mujibu wa kanuni kukamilisha hatua hiyo.
Fomu hizo zinazopatikana ofisi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam, zilianza kutolewa juzi Julai 3, 2017 na mwisho ni Julai 7,
mwaka huu.
“Wanaojitokeza wachache. Wengine wanadai
hawafahamu zilizo ofisi za DRFA. Tunatoa wito wajitokeze kwa wingi
kuwania nafasi mbalimbali,” amesema Mambosasa
.
.
Nafasi
zilizotangazwa kuwaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu,
Katibu Msaidizi, Mweka Hazina ambao fomu zao zinapatikana kwa Sh 200,000
wakati nafasi za wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya
Utendaji fomu zao zinapatikana kwa Sh 100,000.
UCHAGUZI CHAMA CHA WATAALAMU WA TIBA ZA MICHEZO
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo
(TASMA), kimetangaza Uchaguzi Mkuu wa chama hicho kwamba utafanyika
Agosti 5, mwaka huu katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es
Salaam.
“Wanachama wote wanakaribishwa kushiriki kwa
namna moja au nyingine katika zoezi hili muhimu sana,” amesema
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Leslie Liunda alipokuwa anatangaza ramani ya
mchakato wa uchaguzi huo leo Alhamis Julai 06, 2017.
Amesema:
Mwanachama ye yote anayependa kukiongoza chama hiki anaombwa kuchukua
fomu katika ofisi za Olimpiki Maalumu, zilizoko jirani na Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam kwa ajili ya kugombea nafasi anayoona kuwa anaweza
kuimudu.”
Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina ambao fomu zao
zinapatikana kwa Sh 200,000 wakati nafasi za wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF
na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu zao zinapatikana kwa Sh 100,000.
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}