Sponsor

header ads

Baada ya Lipumba kuwavua ubunge baadhi ya wabunge wa Cuf Maalim seif nae awavua ubunge wengine Akiwemo sakaya

Chama cha Wananchi (CUF), upande wa Katibu
Mkuu, Maalim Seif kimewavua uanachama
wabunge wawili, Magdalena Sakaya na Maftaha
Nachuma.
Kwa mujibu wa uamuzi huo, wabunge hao
wanapoteza sifa ya kuwa wabunge.
Hatua hiyo inahisiwa kuwa ni kulipiza kisasi
baada ya CUF, upande wa Mwenyekiti, Profesa
Ibrahim Lipumba kuwavua uanachama wabunge
8 wa viti maalum na madiwani wawili na hivyo
kupoteza sifa ya kuwa wabunge huku nafasi zao
zikiwa zimechukuliwa na wabunge wengine
waliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC).
Hatahivyo, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
tayari imesema kuwa haitambui maamuzi hayo
ya Maalim Seif.

Post a Comment

0 Comments