Sponsor

header ads

Magunia Ya bangi yaliyokamatwa Arusha ni zaidi ya..>

Na mwandishi  @Judithbitehabari

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, Wilayani Arumeru,
limekamata zaidi ya magunia 400 ya bangi
pamoja na watuhumiwa 14 na pikipiki nne, huku
baadhi ya watuhumiwa wakitelekeza nyumba zao
na kukimbilia porini kufuatia operesheni maalum.
Kamishina Intelijensia Mamlaka ya Kudhibiti na
Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini Bw.
Fredrick Kibute amesema pia wamekamata kiasi
kikubwa cha mbegu za bangi.
Operesheni hiyo ni utekelezaji wa agizo la serikali
la kutokomeza madawa ya kulevya inayofanyika
kote nchini ambapo Wilaya ya Arumeru ni
miongoni mwa wilaya zenye kiwango kikubwa
cha zao la bangi ambalo limekuwa ndio tegemeo
la maisha ya wananchi wengi na licha ya
kufanyika kwa jitihada kubwa za kulidhibiti bado
tatizo ni kubwa.

Post a Comment

1 Comments

Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}