Sponsor

header ads

COSAFA YATOA ZAWADI TAIFA STARS, WACHEZAJI

Baraza la Soka kwa Nchi za Kusini mwa Afrika
(Cosafa) limetoa zawadi ya dola 10,000 kwa
Taifa Stars ya Tanzania baada ya kushinda na
kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya
Castle Cosafa yaliyofanyika mwezi uliopita
nchini Afrika Kusini.
Fedha hizo ni sawa na Sh 22,000,000 ambako
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeamua
fedha hizo kwa mgawanyo sawa, zitolewe kwa
wachezaji wote walioshiriki fainali hizo pamoja
na benchi la ufundi.
Kadhalika Cosafa limetuma fedha za zawadi
kwa wachezaji wa Tanzania ambao walifanya
vema kwenye mchezo mmoja baada ya
mwingine katika mashindano hayo ambayo
yalikuwa na mvutio wa aina yake kwa
mafanikio ya timu ya Tanzania.
Wachezaji hao ni Shiza Kichuya aliyeibuka
Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na
Malawi; Muzamiru Yassin aliyeibuka Mchezaji
Bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola;
Erasto Nyoni aliyeibuka Mchezaji Bora wa
mechi kati ya Tanzania na Mauritius; Elius
Maguri aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi
kati ya Tanzania na Afrika Kusini.
Kipa Bora wa michuano hiyo ni Said
Mohammed aliyezawadiwa moja kwa moja na
Cosafa. Tanzania ilishika nafasi ya tatu nyuma
ya mabingwa Zimbabwe na Zambia iliyoshika
nafasi ya pili. Tanzania iliifunga Lesotho na
kushika nafasi ya tatu.

Post a Comment

0 Comments