Sponsor

header ads

Bunge laijibu chadema hela za wabunge kwa tundu lissu

Ofisi ya Bunge imesema kuwa fedha zilizochangwa na wabunge kiasi cha Shilingi Milioni 43 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu zimetumwa katika akaunti ya Hospitali ya Nairobi mahali anakopatiwa matibabu.
Katika taarifa hiyo, Bunge limesema kuwa fedha hizo zilitumwa Septemba 20, mwaka huu kupitia Benki ya Barclays, Tawi la Hurlringham katika akaunti namba 0451155318 yenye jina la Kenya Hospital Association.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, fedha hizo zingekuwa zimeshatumwa mapema isipokuwa kilichochelewesha ni mawasiliano ili kupata akaunti ya kutuma fedha hizo na taratibu nyingine za malipo nje ya nchi.
Taarifa ya Bunge imekuja baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kunukuliwa leo akisema kuwa sio chama wala familia ya Lissu iliyopokea fedha hizo zinazodaiwa kuchangwa na wabunge.
Aidha, Ofisi ya Bunge inawaomba Watanzania kupitia imani zao kuzidi kumuombea Lissu ili apone haraka na kurejea nchini kuendelea na majukumu yake.
Mhe. Lissu alivamiwa na kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, akiwa nyumbani kwake Area D, Mkoani Dodoma akiwa anatoka Bungeni, ambapo alipatiwa huduma ya kwanza katika Hospitali ya Dodoma kabla ya kusafirishwa usiku wa siku hiyohiyo kwenda Nairobi, Kenya kwa matibabu zaidi.
Siku iliyofuatia wabunge waliazimia kutoa nusu ya posho ya kila mmoja wao ili kuchangia gharama za matibabu ya Lissu, ambapo Spika, Mhe. Job Ndugai alisema jumla zitakuwa Shilingi Milioni 43

Post a Comment

0 Comments