Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Freeman Mbowe amesema mtuhumiwa namba moja katika shambulio la Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu ni Vyombo vya Ulizni na Usalama.
Mbowe amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika Mkutano na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Chadema ikiwa ni mara ya kwanza akitoa taarifa kuhusiana na hali ya Lissu akiwa katika ardhi ya Tanzania na kudai kuwa taarifa za kwamba tukio hilo ni la ujambazi sio kweli kwani hakuna ujambazi wa aina hiyo nchini.
“Tumeongea na vyombo vya uchunguzi vya kimataifa vyote viko tayari kutoa msaada lakini wamesema wanasubiri barua ya Serikali,” ameongeza.
Amesema jumla ya Shilingi Milioni 204 zimekusanywa hadi sasa kwa ajili ya matibabu ya Mhe. Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mwandamizi wa Chadema, na kwamba kati ya hizo, Shilingi Milioni 43 zilizokusanywa kutoka bungeni bado hazijakabidhiwa kwa familia ya Mhe. Lissu.
Amesema kwa namna ambavyo Lissu ameumizwa, atahitaji maombi mengi ya kumrudisha aweze kukaa vizuri na kuna kila dalili ya matibabu yake yakaishia Jijini Nairobi.
Mhe. Lissu alivamiwa na kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mnamo Septemba 7, mwaka huu akiwa nyumbani kwake Area D, Mkoani Dodoma,, ambapo alikimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan Jijini Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya kuhudumiwa huduma ya kwanza katika Hospitali ya Dodoma.
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}