Sponsor

header ads

Habari za usajili ulaya leo jully 26 ulaya nimekuwekea hapa

Inasemekana mshambuliaji wa klabu ya
Barcelona Neymar ameiomba klabu ya PSG
kumnunua Coutinho, Neymar ambaye yuko njiani
kuelekea PSG inasemekana anaaamini
muunganiko wake na Coutinho utakuwa hatari.
Wakati huo huo kiungo huyo wa Liverpool
Phellipe Coutinho inadaiwa kwamba
ameshafanya makubaliano binafsi na klabu ya
Barcelona na kinachosubiliwa ni Liverpool
kukubali ofa ya Barca.
Klabu ya Liverpool inaonekana iko tayari
kumuuza Emre Can kwenda Juventus ambapo
klabu hiyo imeshakubali kitita cha £30m kutoka
kwa miamba hiyo ya nchini Italia.
Kocha Jose Mourinho ameuthibitishia ulimwengu
kwamba bado anahitaji kusajili na safari hii
anataka kununua kiungo mkabaji na
mshambuliaji ambae atacheza kutokea pembeni
ya uwanja
Carlo Anceloti amethibitisha kwamba Renato
Sanchez anaweza kuondoka Bayern Munich na
kusema kwamba anaweza kwenda kukipiga Epl
ambako Manchester United wamekuwa
wakitajwa kumnyatia.

Post a Comment

0 Comments