Sponsor

header ads

USAJILI SIMBA, YANGA NI UTATA, KUMBE MAJINA YA OKWI, AJIBU HAYATAMBULIKI TFF

Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF)
limezikumbusha klabu zote ambazo
zinasimamiwa na shirikisho hilo kuhakikisha
zinamaliza zoezi lake la usajili mapema.
TFF imetoa tamko hilo kupitia kwa Ofisa
Habari, Alfred Lucas kuwa katika timu 16 za
Ligi Kuu ya Tanzania Bara ni mbili pekee ndizo
ambazo zimewasilisha majina yao ya usajili
kuelekea msimu ujao wa 2017/18.
Katika majina ya klabu hizo, Simba na Yanga
siyo miongoni mwao, hiyo inamaana kuwa
kumbe hata wachezaji wao wapya
waliosajiliwa hivi karibuni bado hawatambuliki
ndani ya mfumo wa usajili wa shirikisho hilo.
Baadhi ya wachezaji waliosajiliwa hivi karibuni
ni Emmanuel Okwi kwa upande wa Simba na
Ibrahim Ajibu upande wa Yanga.
Alfred amesema timu 24 za Ligi Daraja la
Kwanza na 24 Ligi Daraja la Pili zinatakiwa
kukamilisha mfumo wa usajili kwa kuwa
imesalia wiki moja tu kabla ya mfumo
kufungwa.
Dirisha la usajili lilifunguliwa Juni 15, mwaka
huu na litarajia kufungwa Agosti 6, mwaka
huu.

Post a Comment

0 Comments