Kocha mpya wa Lipuli FC, Selemani Matola
amezungumza juu ya mikakati yake ya
kuijenga upya timu hiyo ambapo amesema ana
mipango ya kuongeza wachezaji 10 wapya.
Matola ambaye ni kiungo na kocha wa zamani
wa Simba, amesema kuwa usajili huo wa
wachezaji 10 unatokana ripoti ya kocha
aliyepita ambayo aliikabidhi klabuni hapo.
Amesema kutakuwa na wachezaji 10 wapya,
pia walioipandisha timu nao watabaki 10 na
wachezaji watano watapatikana kutokana na
majaribio ambayo wamekuwa wakiyafanya
kikosini hapo.
Hivyo, jumla Lipuli FC itakuwa na wachezaji 25
katika msimu ujao wa 2017/18, lakini amedai
kuwa usajili huo utategemea na mwongozo wa
uongozi wake wa Lipuli FC.
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}