Baada ya ushindi mjini Santa Clara, Kocha Jose
Mourinho wa Manchester United amesifia
Anthony Martial kwa kucheza vizuri lakini akimpa
angalizo kuwa ajitahidi kuhifadhi kiwango
alichoonyesha.
United walishinda kwa mikwaju ya penalti dhidi
ya Real Madrid katika International Champions
Cup baada ya sare ya 1-1. Msimu mzuri wa
nyota huyo wa Ufaransa ulikuwa 2015/16 pale
alipojihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza.
Aidha kiwango kizuri cha mlinda mlango David de
Gea anayewindwa na Los Blancos kwa muda
sasa kinaonyesha bado ataendelea kusalia na
miamba hiyo ya Old Trafford.
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}