Real Madrid ni klabu tajiri yenye mashabiki
wengi kila kona ya Dunia. kuna jarida moja
liliwahi kuripoti kuwa ‘Pitch’ ya Real Madrid ina
thamani kubwa kwani unaweza kuwa
mfanyakazi wa ndani wa klabu ya Real Madrid
hata kwa miaka 10 na usiikanyage ‘Pitch’ hiyo.
Thamani ya Madrid imejengwa na mafanikio
iliyopata timu hii sambamba na wachezaji
wakubwa waliowahi kucheza Bernabeu.
Wachezaji wengi wamekuwa radhi kukaa
kwenye benchi la Madrid na sio kuhama.
Baada ya kuondoka mshambuliaji Alvaro
Morata aliyekuwa anakipiga Real Madrid na
kutimkia Chelsea, Real Madrid imejikuta ikibaki
bila ya mshambuliaji zaidi ya Kareem Benzema.
Cristiano Ronaldo mara kadhaa amekuwa
akicheza kama namba 9 kutokana na uwezo
wake wa kukimbia kupungua ila bado Madrid
kwasasa haina namba 9 wa uhakika zaidi ya
Kareem Benzema. Japo Bale na Ronaldo
wanaweza kucheza namba hii ila mrithi wa
Morata bado anahitajika pale Bernabeu.
Kutokana na hili wachambuzi mbalimbali
wamekuwa wakitaja baadhi ya wachezaji ambao
huenda mmoja wao akarithi nafasi ya Alvaro
Morata. Hapa chini ni baadhi ya majina
yanayopendekezwa na wengi kabla ya dirisha
kufungwa.
Kylian Mbappe ni Mshambuliaji hatari
anayekipiga AS Monaco ya nchini Ufaransa.
Mbappe amekuwa akitajwa mara kadhaa
kujiunga na Madrid kwa ada ya kuvunja rekodi
ya usajili Duniani. Inawezekana huyu akawa
mrithi sahihi kwani umri mdogo alionao Mbappe
unaweza kumpa mafanikio pale Madrid. Mbappe
ni mshambuliaji mchanga kwani katika michezo
58 aliyoichezea Monaco ameweza kufunga
magoli 27. Anaweza kucheza bila presha hata
kama akiwa anatokea benchi.
Madrid inahitaji mshambuliaji ambaye hana
presha ya kuanza kama ilivyo kwa Morata kwani
kwa sasa hakuna mshambuliaji sokoni mwenye
kiwango cha kuanza pale Madrid zaidi ya Costa.
Mbappe anaweza kumrithi Morata na hii ni
kutokana na kutokea Ligue 1, ligi ambayo hata
mshambuliaji wa sasa Kareem Benzema
katokea. Miaka 18 aliyonayo inatosha kuwa
bidhaa nzuri kwa Madrid katika kutafuta mrithi
wa Alvaro Morata ambaye alikuwa hapati nafasi
ya kuanza.
Lucas Perez ni mshambuliaji wa Arsenal
ambaye majaaliwa yake hayajulikani baada ya
usajili wa Lacazette pale Emirates. Lucas Perez
anaweza kuwa mrithi sahihi wa Morata hasa
kutokana na uzoefu wake wa kucheza ligi kuu
ya Hispania. Akiwa Deportivo La Coruña kabla
ya kuhamia Arsenal, Perez alicheza michezo 36
na kufunga mara 17. Uraia wake unampa nafasi
ya kurejea Hispania licha ya umri wake kuwa
mkubwa. Kutopata nafasi Arsenal kunawapa
Madrid nafasi ya kumsajili.
Timo Werner wa RB Leipzig inayocheza
Bundesliga, anaweza kuwa mrithi sahihi wa
nafasi hii. Endapo ningekuwa Zidane
nisingechelewa hata punde kutuma ofa pale
Leipzig. Werner ni chipukizi hatari ambaye
amefanya makubwa kwenye michuano ya
mabara iliyomalizika kwa timu yake ya
Ujerumani kutwaa ubingwa. Miaka 24 aliyokuwa
nayo inatosha kumfanya asiwe na presha ya
kuanza pale Madrid. Chipukizi huyu anaweza
kufunga kwani katika michezo 43 amefunga
mara 26.
Diego Costa wa Chelsea anaweza pia kwenda
kumrithi Morata japo hatopenda kusubiri nyuma
ya Benzema. Maelewano mabovu baina yake na
kocha wake yamefanya awe njia panda hasa
baada ya kuambiwa hatakiwi na Conte. Japo
anatamani kurejea Atletco ila sidhani kama
atajiuliza mara mbili endapo Real watatuma ofa
Chelsea. Costa ni Mshambuliaji mwenye uwezo
mkubwa zaidi hata ya Alvaro Morata na huenda
akaisaidia Madrid endapo akipata nafasi ya
kusajiliwa.
Andrea Belotti aliyezaliwa 20 December 1993
anaweza kuwa mshambuliaji wa mwisho kwenye
listi hii. Umri wake, klabu anayocheza na
kiwango chake haviwezi kumfanya akatae
kwenda Madrid kurithi nafasi ya Morata. Belotti
hatochukia kusubiri baada ya Benzema na
Ronaldo. Mshambuliaji huyu amekuwa akitajwa
kuondoka Torino katika dirisha hili na huenda
akahamishia makazi yake jijini Madrid kama
mambo yatakwenda sawa.
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}