Prof.Ibrahim Lipumba (kushoto) pamoja na Julius
Mtatiro.
Wakati sakata la Chama cha Wananchi (CUF)
likiendelea kuchukua sura mpya baada ya Spika
wa Bunge, Job Ndugai kukiri kupokea barua ya
kufukuzwa wabunge nane wa CUF na Ofisi ya
Bunge kutangaza kuwa nafasi hizo ziko wazi na
kuiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),
kwa hatua stahiki, Kiongozi anayeegema upande
wa Katibu Mkuu, Maalim Seif, Julius Mtatiro
ameibuka tena na kutoa ya moyoni kuhusiana na
matukio yote hayo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mtatiro
ameandika yafuatayo;
“HATUA ZA BUNGE, LIPUMBA NA MSIMAMO
WANGU!
1. Juzi Jumatatu Lipumba na Sakaya
walimuandikia Spika wa Bunge kumjulisha kuwa
“Baraza Kuu la CUF” (feki) limewafukuza
uanachama Wabunge 8 wa Viti Maalum wa CUF.
(Spika alishaandikiwa na Katibu Mkuu
kumjulisha kuwa Baraza Kuu halali la CUF ni
lile lililochaguliwa mwaka 2014 na muda wake
utaisha mwaka 2019 na Baraza hilo halali ndilo
lililomfukuza Lipumba).
2. Jana, Jumanne, Ofisi ya Bunge ilitoa taarifa
kwa umma kuujulisha kuwa imepokea
maelekezo kutoka kwa Sakaya na Lipumba
kuwa wabunge hao 8 si wanachama na Ofisi
hiyo ikaeleza kuwa bado inatafakari hatua za
mwisho za kuchukua.
3. Leo Jumatano, Ofisi ya Bunge imetangaza
uamuzi wake, kwamba inakubaliana na
maelekezo ya Lipumba na Sakaya na kuwa
imewavua wabunge hao 8 ubunge wao wa Viti
Maalum, na kuwa imeiandikia Tume ya Taifa ya
Uchaguzi kuijulisha kujaza nafasi hizo zilizo
wazi.
_____#___#______________________________
Ukiitizama hii kasi ya maamuzi ya vyombo muhimu
vya nchi juu ya jambo kubwa kama la kuwafukuza
wabunge tena kwa kuletewa taarifa na mtu ambaye
alishafukuzwa uanachama huku akiwa haungwi
mkono na vikao halisi na halali vya Chama;
unaweza kutambua kuwa Lipumba ni mradi
muhimu wa kuleta Viwanda Tanzania .
Ndani ya siku 3 Serikali nzima, bunge,
vinakimbizana kuchukua hatua za kipuuzi na bila
aibu kwa kasi ya ndege ya kivita! Tanzania kwa
sasa haina sheria wala taratibu, ni kutekeleza tu
maelekezo ya wakubwa!
_________________________________________
TUKO IMARA ZAIDI
Nataka kuwaeleza wanachama na watanzania wote,
kwamba viongozi wa chama wanakutana kuendelea
kuchukua hatua.
Tunajua kuwa Vyombo vya Serikali hivi sasa
vinafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa aidha CUF
inamkubali “MSALITI” Lipumba kuwa Mwenyekiti
wake, au CUF isambaratike. Na suluhisho la hali
hii haliwezi kuwa kukaa chini na MSALITI.
Mnapopambana na WASALITI WALIOKUBUHU na
wako ndani ya nyumba yenu, vita yake siyo ndogo.
Lakini mimi binafsi ni muumini mkubwa wa HAKI
na UKWELI. Naamini kuwa CUF itavuka misukosuko
hii.
Kwa jicho moja wapo watu wanachekelea na
kudhani kadhia hii ni ya CUF tu, mimi natizama hali
hii kama Mapambano ya Dola ya kuhakikisha vyama
mbadala vinaongozwa na wasaliti ili Dola iendelee
kuwatumia kuzamisha demokrasia na ushindani wa
kisiasa nchini.
Dola ikifanikiwa kuisambaratisha CUF, vyama
vingine vya upinzani havitakuwa salama, taasisi
zingine za kiraia hazitakuwa salama pia.
Anayeyatizama mapambano haya kama vita ya
ndani ya CUF hajaisoma dunia – haya ni
mapambano makubwa, dhidi ya demokrasia ya
Tanzania.
Mimi ni mwanademokrasia imara na sitayumbishwa
na WASALITI. Kumkubali Lipumba na genge lake
itakuwa na maana ya kuiua CUF moja kwa moja
Tanzania Bara, maana alipojaribu kukimbia mwaka
2015, ndipo CUF iliibuka na kuwa chama imara
mara 10 Tanzania bara. Na kurudishwa kwake kwa
nguvu kunakofanywa na dola ni mkakati wa
kuimaliza CUF na suluhisho lake haliwezi kuwa
CUF kumtambua Lipumba.
Hata DOLA ikifanya nini, LIPUMBA
ameshadharaulika na hawezi kuisaidia tena dola hii
yenye upofu. Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. Seif
Sharif Hamad na viongozi wa chama wanaendelea
na hatua mbalimbali muhimu na mtajulishwa
Vita imeshapanuka, sasa ni LIPUMBA, OFISI YA
MSAJILI WA VYAMA, RITA, BUNGE, NEC, IKULU,
USALAMA WA TAIFA na CCM. Kundi lote hilo
linaamini kuwa bila kumrudisha Lipumba
halitaweza kuidhibiti CUF. Sisi viongozi tuko imara
sana na tunaamini kuwa HAKI huweza
kucheleweshwa tu!
We shall OVERCOME this! More Stable! And more
Vibrant!.”
@ BossanDingy
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}