Baadaye ya kuachiwa kwa dhamana
Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu muda
huu anaongea na waandishi wa habari.
1.==>>Tundu Lissu "Hakuna gereza
litakalotunyamazisha. Mwambieni Magufuli,
tutanyamaza tukiwa wafu. Wafu huwa
hawasemi"
2=>Tundu Lissu "wanataka tunyamaze ili
waendeshe nchi hii wanavyotaka wao, Taifa hili
ni la mfumo wa vyama vingi, tunayo haki ya
kufanya mikutano, tunayo haki ya kufanya
maandamano na tunayo haki ya kutoa maoni
yetu. Kwa msingi huo hakuna wa
kutunyamazisha, nchi hii siyo mali ya mtu
binafsi.”
3=>Tundu Lissu "naomba niweke wazi kabisa.
Hakuna gereza, wala mahabusu, wala polisi,
wala usalama wa taifa, wala Magufuli na wala
mtu yeyote atakayetunyamazisha. Narudia.
“Hatutakubali kunyamazishwa. Kwa sababu,
tukinyamaza kwa kuogopa mahabusu, tukaogopa
magereza, tukaogopa mabomu ya mapolisi,
tukanyamaza. Nchi hii, inaangamia.”
4=>Tundu Lissu "Hatutaogopa kunyamazishwa na
mtu yeyote kwa sababu tukinyamaze nchi hii
inaangamia"
5=>Tundu Lissu Njia rahisi ya kwenda mbinguni ni
kupinga uonevu.
"Mwambieni Magufuli tutanyamaza tukiwa Wafu"
6=>"Tundu Lissu Siku yoyote ukimatwa na Jeshi
la Polisi na kuambiwa wanaenda kukupima
mkojo waambie mimi sitaki kwa sababu Jeshi la
Polisi hawana mamlaka hayo kisheria. Tundu
Lissu
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}