Sponsor

header ads

Mbwana samatta Aifungia gori Krc genk mechi ya kwanza ya ligi

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa
Stars Mbwana Samatta leo Jumamosi ya July 29
ameingia uwanjani kuichezea timu yake ya KRC
Genk katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi
Kuu Ubelgiji msimu wa 2017/18 dhidi ya
Waasland Beveren .
KRC Genk leo imecheza game yake ya kwanza
katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya
Waasland Beveren na kulazimishwa sare ya
kufungana magoli 3-3, magoli ya Genk
yakifungwa na Jose Naranjo dakika ya 70,
Mbwana Samatta dakika ya 80 na dakika ya 82
Shrivjers akafunga goli la mwisho.
Magoli ya Waasland yamefungwa na Olivier
Myny dakika ya 45, Zinho Gano dakika ya 47 na
90, sare hiyo sasa inakuwa ni sare ya pili
mfululizo kwa timu hizo toka zilipokutana mara
ya mwisho February 7 2017 na kutoma sare
tasa, Genk na Waasland zote baada ya sare ya
leo zinashika nafasi ya nne zikilingana kila kitu.

Post a Comment

0 Comments