Jumla ya watu 20 wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma kuwa walikutwa wakifundishana namna ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
Wanawake 12 pamoja na wanaume 8 walikamatwa wakiwa katika hoteli moja ambako walikuwa wakupatiwa elimu juu ya ugonjwa wa UKIMWI.
Mapema mwaka huu, mamlaka ilivipiga marufuku vituo binafsi vya matibabu kutojihusisha na utoaji wa huduma zinazohusiana na ugonjwa wa Ukimwi kwa madai kuwa zinachochea mapenzi ya jinsia moja.
Kwa Tanzania mapenzi ya jinsia moja ni kosa la jinai na inaweza kukupelekea kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 30 jela.
Kamanda wa Polisi wa mkoa Hassan Ali Nasri alieleza kuwa watu hao wanahusishwa na mapenzi ya jinsia moja na wanawashikilia huku uchunguzi ukiendelea.
‘Polisi haiwezi kuufumbia macho vitendo vya namna hii.’
Jana Ijumaa, Naibu Waziri wa Afya Hamis Kigwangala alilieleza Bunge kuwa wanapambana kwa nguvu zote dhidi ya makundi ya wale wanaounga mkono mapenzi ya jinsia moja katika nchi ya Tanzania.
Mnamo mwaka 2016 serikali ilizuia uingizwaji na uuzwaji wa vilainishi huku Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akieleza kuwa vinahamasisha uwepo wa mapenzi ya jinsia moja yanayochangia ongezeko la ueneaji wa virusi vya ukimwi.
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}