Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), imefanya mabadiliko kidogo ya timu
zilizo kwenye makundi ya ‘A’ na ‘B’ katika Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania Bara
iliyopangwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Timu ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Polisi
Morogoro FC ya Morogoro iliyokuwa kundi ‘A’
sasa itakuwa Kundi ‘B’ wakati Mshikamano FC
ya Dar es Salaam iliyokuwa Kundi ‘B’ sasa
itacheza mechi mechi zake katika Kundi ‘A’.
Kwa msingi huo, makundi ya Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) kwa timu 24 zilizogawanywa
katika makundi matatu yenye timu nane kila
kund, zitakazochuana msimu huu wa 2017/18
kuwania nafasi tatu muhimu za kupanda
daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara (VPL) msimu wa 2018/19 yatakuwa hivi:-
Kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon,
Ashati United, Friends Rangers, Mshikamano
za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United
za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na
Mvuvumwa ya Kigoma.
Kundi ‘B’ zitakuwa timu za itakuwa na timu za
Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya
Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mbeya
Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa,
Polisi Dar za Dar es Salaam na Polisi
Morogoro na Mawezi Market ya Morogoro.
Kundi ‘C’ ina timu za Alliance School, Pamba
na Toto African za Mwanza, Rihno Rangers ya
Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya
Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT
Oljoro ya Arusha.
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}