Sponsor

header ads

Tanzania yashuka viwango FIFA

Viwango vya kila mwezi vya ubora katika kandanda vinavyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), vinaonyesha Tanzania imeshuka nafasi tano kutoka 120 mwezi uliopita hadi 125.
Ujerumani imepanda kileleni na kuibwaga Brazil huku nafasi ya tatu ikishikwa na Ureno iliyopanda kwa nafasi tatu. Argentina imeshika nafasi ya nne ikianguka nafasi moja huku Ubelgiji ikipanda nafasi ya nne na kushika nafasi ya tano.
Poland, Uswisi, Ufaransa, Chile na Colombia zinafunga kumi bora ya dunia. Kwa bara la Afrika nchi ya kwanza ni Misri ambayo imeshika nafasi ya 30 duniani, ikifuatiwa na Tunisia (31), Senegal  (33), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (42), Nigeria (44), Cameroon (45), Burkina Faso (49), Ghana (52), Ivory Coast (54), Morocco (56).
Algeria imeshika nafasi ya 11 barani Afrika huku ikiangukia nafasi ya 62 duniani ikiwa imeanguka nafasi 14. Uganda imepanda nafasi mbili juu ikishika nafasi ya 71 duniani. Kenya imeshika nafasi ya 88 ikianguka nafasi sita.

Post a Comment

0 Comments