Siku chache baada ya kuteuliwa kuwa
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally
amesema ni mpenzi mkubwa wa nyimbo
za msanii wa Bongo Fleva, Ally Kiba.
Akizungumza na MCL Digital katika
mahojiano maalum, Dk Bashiru amesema
hata dereva wake anafahamu kuwa
anampenda msanii huyo na kwamba
akiingia katika gari hupiga nyimbo za Ali
Kiba hadi mwisho wa safari yake.
“Kwa upande wa wasanii, mimi napenda
sana nyimbo za Ally Kiba, dereva wangu
ameshajua nikiingia kwenye gari anapiga
tu nyimbo zote zinafululiza mpaka
nashuka,”amesema.
“Ila sijui kama Ali Kiba ni mwana CCM
ama la. Sitajali kama ni mwana-CCM
kwasababu nyimbo zake zinafanya kazi
niliyoisema ya kujengea watanzania hari
ya kujiamini.”
Amesema wasanii wamewapamba sana
Watanzania kitaifa na hata kimataifa na
kwamba hata nafasi ya waafrika katika
tasnia hiyo iko juu jambo ambalo limeleta
heshima.
“Mimi sijali mahadhi kama ni ya kigeni
ama kikabila kama ni ya Kiswahili kama
ni taarabu ili mradi una maudhui kuna
ujumbe. Na ndani ya CCM sisi
tunadhamini sana sanaa na tunakitengo
maalum ambacho kipo chini ya uenezi
kinaongozwa na Polepole (Katibu wa
Itikadi na Uenezi Humprey
Polepole) ,”amesema.
Amesema ndani ya chama wana kikundi
cha TOT na Vijana Jazz ambavyo
anataka viimarike na kufanya kazi ya
kukitangaza chama kuhusu mazuri ya
nchi.
Amesema bila ya kuwa na michezo, Taifa
halitatambuliwa, umoja hautokuwepo na
hata hatua za maendeleo
hazitatambuliwa na mataifa mengine.
Amesema CCM wanamiliki viwanja lakini
bado haviko katika hali nzuri na kwamba
atajaribu kuwekeza na kuvifufua ili viwe
na mchango katika jamii.
Bofya kupakua
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}