Aliyekuwa Mgombea Urais nchini Kenya, Raila
Odinga ametangaza kutogombea tena nafasi ya
Urais baada ya kubwagwa na Uhuru Kenyatta
katika Uchaguzi uliofanyika Agosti 8, mwaka
huu.
Hata hivyo Raila hakukubaliana na matokeo hayo
na kuwataka wafuasi wake kutoenda kazini siku
ya jana ili kupinga matokeo hayo lakini watu hao
walipuuza agizo hilo na kuendelea na shughuli
zao kama kawaida.
“Tutauonyesha ulimwengu ulivyochezewa,”
amesema Odinga.
Bwana Odinga ambaye alikuwa akiwania urais
kwa mara ya nne pia amesema hatowania tena
urais na kwamba anawataka Wakenya kujua
kilichofanyika wakati wa uchaguzi huo.
“Sio swala la kuwa mbifansi, Sio swala kuhusu
Raila Odinga, Sitawania urais tena……tunataka
Wakenya kujua kile kilichofanyika, na kile
ambacho ulimwengu haujui kinafanyika,”
amesisitiza.
Bwana Odinga amedai kwamba wadukuzi
waliingilia kompyuta za tume ya Uchaguzi na
kuweka hesabu ambazo zilimpatia ushindi rais
Uhuru Kenyatta.
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}