Rais Mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta
ameruhusu maandamano ya amani ya kupinga
ushindi wake alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa
Agosti 8, mwaka huu.
Hatahivyo, licha ya ruhusa hiyo, Kenyatta
amewataka polisi kujizuia kutumia nguvu kubwa
na badala yake watoe ulinzi wakati wa
maandamano hayo, lakini akaonya kuwa Serikali
haitavumilia watakaoharibu mali za umma.
Tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi,
kumekuwa na vurugu katika baadhi ya maeneo
nchini Kenya yakipinga ushindi wa Kenyatta huku
upinzani chini ya Mwamvuli wa NASA na
aliyekuwa Mgombea Urais wake, Raila Odinga
ukitangaza kutokubali matokeo hayo na kudai
kuwa ni matokeo ya tume ya uchaguzi
yasiyoakisi kura halisi za Wakenya.
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}