Sponsor

header ads

Trump amshukuru putin kuwafukuza wamarekani Nchini Urusi

Rais, Donald Trump amemshukuru mwenzake wa
Urusi, Rais Vladimir Putin kwa kuwaondoa
takribani wafanyakazi 755 wa Ubalozi wa
Marekani nchini Urusi.
Urusi ilifikia uamuzi wa kuwatimua
wanadiplomasia hao baada ya Marekani
kuiwekea vikwazo nchi hiyo kufuatia tuhuma za
kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani mwishoni
mwa mwaka 2016.
“Ningependa kumshukuru kwa sababu hata sisi
tunajaribu kupunguza wafanyakazi wetu,
namshukuru sana kwa kuwafukuza watu wengi
kiasi hicho,” amesema Trump.

Post a Comment

0 Comments