Sponsor

header ads

Jaribio la kifaa cha kuwalinda wanawake dhidi ya ukwimi lanu

Watafiti nchini Marekani wamesema kuwa jaribio
ambalo vijana wa kike walitumia mpira wa
mviringo kujilinda na virusi vya HIV, limefanikiwa.
Wasichana hao walitumia mviringo wa plastiki
uliowekwa dawa za kujilinda na ugonjwa wa
ukimwi, ambao ulibadilishwa kila mwezi katika
kipindi cha miezi sita.
Jaribio hilo ni mojawapo ya mipango ya
kutengeneza kifaa ambacho wanawake
watatumia kujilinda dhidi ya maambukizi ya HIV
na kuondoa utegemezi kwa wanaume kuvaa
mipira ya kondomu.
Watafiti hao wamesema kuwa wanafurahi
kwamba wasichana waliotumia mviringo huo
wameupenda.
Wanawake na wasichana walio kati ya umri wa
miaka 15-24 wanadaiwa kuwa sehemu kubwa ya
maambukizi ya HIV duniani huku takriban
wanawake 1000 huambukizwa virusi hivyo kila
siku kusini mwa Jangwa la Sahara Barani Afrika.
Utafiti zaidi wa mpira huo wa mviringo
unatarajiwa kufanywa kwa vijana barani Afrika.

Post a Comment

0 Comments