Sponsor

header ads

Laurent Blanc-- Kumung'oa Verrati Psg ni Ngumu

Kocha wa zamani matajiri wa Ufaransa Paris
Saint Germain (PSG), Laurent Blanc amesema
itakuwa vigumu kwa kiungo wake Marco Verratti
kuondoka na kwenda Barcelona.
Iliripotiwa mara kadhaa kuwa kiungo huyo yupo
mbioni kutimka Paris na kutua Camp Nou lakini
mpaka sasa inaonekana PSG hawana nia ya
kumuuza kiungo huyo. Blanc ambaye alimnoa
nyota huyo wa zamani wa Pescara ya Italia
amesema haoni nafasi ya Verratti akitoka kwa
miamba hiyo.
“Sijui nini kitatokea kwa Verratti. Marco Verratti
ni mchezaji muhimu sana kwa PSG, ana kila kitu
na PSG watafanya kila wanaloweza kuendelea
kubaki naye,” alisema kocha huyo wa zamani
mwenye miaka 51.
Verratti aliachana na wakala Donato Di Campli na
kujiunga na Mino Raiola hivyo kuwa miongoni
mwa nyota wengine walio mikononi mwa wakala
huyo, wengine ni Paul Pogba, Romelu Lukaku,
Henrikh Mkhitaryan na Zlatan Ibrahimovic.
Nyota huyo wa Italia atakuwamo katika mikono
ya matajiri hao hadi mwaka 2021. Msimu uliopita
Verrati alicheza mechi 43 wakati PSG ilipovuliwa
ubingwa na AS Monaco na alikuwamo wakati
PSG ikipokea kichapo cha aibu katika hatua ya
16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Post a Comment

0 Comments