Sasa unaweza kusema matarajio ya Arsenal
kutwaa taji la Ligi Kuu England ni ndoto ambayo
haielezeki kwa wachezaji waliowahi kupita hapo
na waliopo sasa, mashabiki na wapenzi wa klabu
hiyo. Umemsikia Jamie Vardy anachosema?
Nyota huyo wa Leicester City anasema hajutii
hata kidogo pale alipowakatalia Arsenal kutaka
saini yake.
Anayasema hayo yakiwa yamebaki majuma
kadhaa kuanza kwa mbio za ubingwa wa PL
msimu wa 2017/18 huku Mbweha hao
wakijiandaa kuanza na Washika Bunduki wa
London. Vardy anaamini kuwa bado ana furaha
kuendelea kusalia jijini Leicester.
“Sijutii hata kidogo. Nimefanya maamuzi
makubwa kadhaa katika maisha yangu, yakiwamo
ya kutwaa taji, kushuka daraja na kumaliza
katikati ya msimamo ya ligi, nani ajuaye kuwa
msimu ujao utakuwa mzuri. Hebu tusubiri na
tuone mipango ya klabu inavyotutaka tumalize
nasi tutawekeza kila kitu hapo,” alisema nyota
huyo mwenye miaka 30.
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}