Kocha wa Leicester City, Craig Shakespeare
amewaeleza Arsenal kuwa kiungo wake Riyad
Mahrez yupo tayari kuanza mchezo wa leo
Ijumaa.
Leo ndiyo siku ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya
England ‘Premier League’ kwa mchezo mkali
kati ya Arsenal dhidi ya Leicester City kwenye
Uwanja wa Emirates.
Awali, Arsenal walikuwa wakimtaka kiungo
huyo raia wa Algeria na Leicester
wakatangaza kuwa hawawezi kumuuza, lakini
mwanzoni mwa msimu huu walimtaka tena
ingawa anawaniwa kwa nguvu kubwa na Roma
ambao walipeleka ofa ya pauni milioni 32,
ikakataliwa.
“Sina jambo lolote ambalo linaweza kunizuia
kumuanzisha, naweza tu kuzungumza jinsi
timu yangu itakavyocheza, lakini hakuna hofu
juu ya yeye kuanza.
“Najua kuwa Arsenal walikuwa wanamtaka
lakini hapa yupo kazini na naamini kuwa
ataonyesha kiwango cha juu kwa kuwa yupo
vizuri kiakili.
“Hatujagoma kumuuza ingawa ni hadi
tutakapopata dili sahihi kabisa, lakini
ikishindikana basi atabaki hapa,” alisema
kocha huyo.
Huu utakuwa mchezo wa kwanza mkubwa wa
Arsenal baada ya wikiendi iliyopita kucheza
mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea na
kushinda kwa penalti 4-1, baada ya sare ya
bao 1-1 ndani ya dakika 90.
0 Comments
Comments
[download bo chart app bit.ly/pakuabochartapp}