Sponsor

header ads

Wamiliki wa Liverpool watoa neno kuhusu kuizwa kwa Countinho

Kampuni ya Fenway Sports Group ambao
ndiyo wamiliki wa Klabu ya Liverpool, wametoa
tamko kuhusu tetesi za usajili wa mchezaji
wao, Philippe Coutinho anayewaniwa na
Barcelona.
Liverpool imekuwa katika presha kubwa
kutokana na mchezaji huyo kuwania na
wababe hao wa Hispania lakini Liverpool
wamekataa dau la kumuuza mara tatu.
Awali Barcelona ilikuwa tayari kutoa pauni
72m ili imsajili, baadaye ikatoa pauni milioni
80 na kisha pauni milioni 90 lakini zote hizo
zimekataliwa na Kocha wa Liverpool, Jurgen
Klopp ambaye amesema kuwa Coutinho bado
yumo kwenye mipango yake.
Wamiliki hao wametoa tamko la maandishi
kuwa hawana mpango wa kumuuza Coutinho
kwa kiwango chochote kile.
Wamesema Hivyo baada ya kuwepo kwa
taarifa kuwa Barcelona wanataka kuweka
pauni pauni milioni 100 ili kuongeza ushawishi
wa kumsajili Coutinho.

Post a Comment

0 Comments