Sponsor

header ads

Simba yampotezea Mzee Kilomoni waendelea na mchakato wa kumpa timu Mo Dewj

By bossan dingy

Wakati wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa
Klabu ya Simba wakiwa wanajipanga kwenda
mahakamani kuzuia mikutano ya Klabu ya
Simba, upande wa pili uongozi wa klabu hiyo
umeonyesha kutojali na unaendelea na
mchakato wa kujiandaa kwa ajili ya msimu
ujao na mabadiliko ya kikatiba kama kawaida.
Kupitia taarifa yao kwa vyombo vya habari
ambayo Simba imeitoa, imeeleza juu ya
mchakato wa kuendeleza mabadiliko
kuendelea kama kawaida bila kujali kitisho
hicho cha Baraza la Wadhamini wakiongozwa
na mzee Kilomoni.
Mabadiliko hayo yanahusisha uendeshaji wa
klabu ambapo kumekuwa na taarifa kuwa
Mohamed Dewji ‘Mo’ ni mmoja wa
wanaowania nafasi ya kuimiliki Simba endapo
kutafafanyika mabadiliko ya kikatiba kuhusu
uendeshaji na umiliki wa klabu hiyo.
Taarifa kamili ya Simba hii hapa:
TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Simba inayo furaha kubwa ya kuanza
mchakato wa elimu ya mabadiliko ya muundo
wa klabu.
Muundo huo unatokana na mabadiliko ya katiba
yaliyofanywa na wanachama na kusajiliwa na
msajili wa vilabu nchini.
Kamati inayoratibu zoezi hilo itaanza kazi hiyo
ya utoaji elimu jumamosi hii, kwa kukutana na
Wenyeviti wa matawi, kwenye Semina
itakayofanyika Makao makuu ya klabu, mtaa
Msimbazi kuanzia saa tatu na nusu.
Semina hiyo ya tarehe tano, itatanguliwa na
nyingine zitakazofanyika kwenye wilaya zote za
mkoani Dar es salaam, zikuhusisha wanachama
wote kutoka kwenye wilaya hizo.
Pamoja na semina hizo, kamati hiyo pia itatoa
elimu kupitia Televisheni,vituo vya Redio na
Magazeti,lengo likiwa kila mwanachama wa
Simba awe na ufahamu mpana kabla ya
mkutano maalum wa katiba wa tarehe ishirini ya
mwezi ujao.
Ratiba kamili ya semina nyingine tutaitoa
mwishoni mwa wiki hii.
IMETOLEWA NA HAJI MANARA
MKUU WA HABARI SIMBA SC *SIMBA NGUVU
MOJA*

Post a Comment

0 Comments